Monday, 11 April 2016

VIONGOZI WA SONU WACHUNGUZWE KUHUSIANA NA MIHADHARATI -MUTUTHO


Mwenyekiti wa NACADA John Mututho

 Ben Kirui

Mwenyekiti wa shirika la kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini Nacada John Mututho anawataka viongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wafanyiwe uchunguzi kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya na uuzaji wa dawa hizo chuoni humo.
Mututho kwa mara nyingine amekariri kwamba uuzaji wa dawa za kulevya katika chuo kikuu cha Nairobi umekithiri mno.
Mututho ameonekana kukerwa sana na picha inayoonyesha mwenyekiti wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi Babu Owino akiwa na bunduki na kuitaka polisi kuchunguza alikopata bunduki hiyo Babu Owino.

1 comment:

Anonymous said...

Babu Owino isn't above the law...atuambie gun alitoa wapi..Joho aliitishwa zake naye pia yeye arejeshe